Uvimbe wa fibrosisi hauna tiba.[3] Maambukizi ya mapafu hutibiwa kwa antibiotiki ambazo zinaweza kudungwa ndani ya mishipa, kuvutwa kwa mapua, au kunywewa. Wakati mwingine antibiotiki ya azithromycin hutumika kwa muda mrefu. Kiowevu cha chumvi kilicho na ukolezi wa juu na salbutamol pia inaweza kutumika. Upandikizaji mapafu unaweza kutekelezwa ikiwa utendakazi wa mapafu utaendelea kuzorota. Ubadilishaji vimeng'enya vya wengu na nyongeza ya vitamini inayoweza kuyeyuka kwenye mafuta pia ni muhimu, hasa kwa watoto. Ingawa hakuna ushahidi wa kutosha, watu wengi hutumia mbinu ya kufungua njia ya pumzi kama vile fiziotherapi ya kifua.[1] Wastani wa matarajio ya urefu wa maisha ni kati ya miaka 37 na 50 katika mataifa yaliyostawi.[6] Matatizo ya mapafu husababisha vifo kwa asilimia 80 ya watu.[1]